Monday, February 20, 2023

 ZAIDI YA  WANAJESHI 50 WA SERIKALI WAUAWA KATIKA SHAMBULIO LA BURKINA FASSO

Taarifa kutoka duru za habari za shirika la habari la uingereza BBC zinasema kuwa,Jeshi la nchini Burkina Faso limesema kuwa zaidi ya wanajeshi 50 waliuawa katika shambulio lililofanywa na watu wanaodhaniwa kuwa wanamgambo wa kiislamu, kaskazini mwa nchi hiyo siku ya Ijumaa.

Katika taarifa yake, imeripotiwa kuwa maiti 51 zimepatikana hadi sasa huku askari kadhaa bado hawajulikani walipo na askari watatu waliojeruhiwa wametolewa katika eneo la tukio.

Siku ya Jumatatu, Jeshi lilisema kuwa askari wanane walifariki katika kile ilichotaja kuwa mapigano makali katika jimbo la Oudalan.

Na kudai kuwaua zaidi ya washambuliaji 100, ingawa idadi hiyo haijathibitishwa.

Mwaka huu kumeshuhudiwa kuongezeka kwa mapigano kaskazini mwa Burkina Faso, huku zaidi ya vifo 100 vimeripotiwa katika wiki sita za mwanzo wa mwaka.

Kushindwa kukomesha umwagaji damu kulisababisha mapinduzi mawili mwaka jana na kumalizika kwa ujumbe wa kijeshi wa Ufaransa nchini humo.

Tukio hili liliripotiwa wakati Ufaransa ikiadhimisha rasmi mwisho wa operesheni zake za kijeshi nchini humo ambapo wanajeshi wa Ufaransa wamekuwa huko tangu mwaka 2015 kusaidia kupambana na wanamgambo.

 RAIS WA MAREKANI AFANYA ZIARA UKRAINE

Duru za habari kutoka shirika la habari za Al jazeera zimeeleza kuwa Rais wa Marekani Joe Biden yuko nchini Ukraine kufanya ziara rasmi kabla ya kukamilika mwaka mmoja toka Urusi kuivamia nchi hiyo Februari 24,2022. Hta hivyo haijafahamika mara moja kuwa lengo kuu la ziara hiyo ni nini, tutaendelea kuwapasha habari kadri zitakavyopatikana


 

 TETEMEKO LA ARIDHI LA UTURUKI NA SYRIA 

Tetemeko la ardhi lililotokea juma lililopita limeripotiwa kugharimu maisha ya zaidi ya watu 45,000 mpaka sasa. Hayo yameelezwa na shirika na habari la kimataifa la Al jazeera hivi punde

 

 ZAIDI YA  WANAJESHI 50 WA SERIKALI WAUAWA KATIKA SHAMBULIO LA BURKINA FASSO Taarifa kutoka duru za habari za shirika la habari la uingereza...