ZAIDI YA WANAJESHI 50 WA SERIKALI WAUAWA KATIKA SHAMBULIO LA BURKINA FASSO
Taarifa kutoka duru za habari za shirika la habari la uingereza BBC zinasema kuwa,Jeshi la nchini Burkina Faso limesema kuwa zaidi ya wanajeshi 50 waliuawa katika shambulio lililofanywa na watu wanaodhaniwa kuwa wanamgambo wa kiislamu, kaskazini mwa nchi hiyo siku ya Ijumaa.
Katika taarifa yake, imeripotiwa kuwa maiti 51 zimepatikana hadi sasa huku askari kadhaa bado hawajulikani walipo na askari watatu waliojeruhiwa wametolewa katika eneo la tukio.
Siku ya Jumatatu, Jeshi lilisema kuwa askari wanane walifariki katika kile ilichotaja kuwa mapigano makali katika jimbo la Oudalan.
Na kudai kuwaua zaidi ya washambuliaji 100, ingawa idadi hiyo haijathibitishwa.
Mwaka huu kumeshuhudiwa kuongezeka kwa mapigano kaskazini mwa Burkina Faso, huku zaidi ya vifo 100 vimeripotiwa katika wiki sita za mwanzo wa mwaka.
Kushindwa kukomesha umwagaji damu kulisababisha mapinduzi mawili mwaka jana na kumalizika kwa ujumbe wa kijeshi wa Ufaransa nchini humo.
Tukio hili liliripotiwa wakati Ufaransa ikiadhimisha rasmi mwisho wa operesheni zake za kijeshi nchini humo ambapo wanajeshi wa Ufaransa wamekuwa huko tangu mwaka 2015 kusaidia kupambana na wanamgambo.
No comments:
Post a Comment